- Rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema ataapishwa Jumanne, Agosti 23
- Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga aliwasili nchini humo jioni ya Jumatatu, Agosti 23 kwa shughuli hiyo
- Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Raila alisema alifurahi sana kushuhudia uhamishaji wa mamlaka bila mgogoro nchini Zambia
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amewasili nchini Zambia kwa ajili ya kuapishwa kwa rais aliyechaguliwa punde Hakainde Hichilema.
Hichilema, ambaye alikuwa kiongozi wa Upinzani wa Zambia na ambaye alikuwa amejaribu bahati yake kuwa rais mara tano alimshinda Edgar Lungu baada ya kupata kura zaidi ya milioni 2.8 kwenye jaribio lake la sita.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii jioni ya Jumatatu, Agosti 23, kiongozi huyo wa ODM alitangaza kuwa amewasili katika taifa hilo la kusini mwa Afrika kwa ajili ya kuapishwa kwa Hichilema shughuli itakayofanyika Jumanne, Agosti 24.
Waziri Mkuu huyo wa zamani alisema kuwa ana furaha sana kushuhudia ukabidhi wa mamlaka bila msukosuko nchini Zambia.
Rais Mtarajiwa wa Zambia Hakainde Hichilema Kuapishwa Agosti 24, 2021
"Nimewasili Lusaka, Zambia kwa hafla ya kuapishwa kesho kwa Rais Mteule Hakainde Hichilema. Itakuwa siku nzuri kwa watu wa Zambia na Afrika kwa jumla kushuhudia uhamishaji wa mamlaka bila mgogoro kama inavyotakiwa na michakato ya kidemokrasia," alisema.
Ujumbe wa pongezi wa Raila
Kama TUKO.co.ke ilivyoripoti, Raila alishangaa jinsi uchaguzi wa Zambia ulivyokuwa wa amani na akawasifu raia kwa kufanikisha zoezi hilo katikati ya janga la COVID-19.
"Uchaguzi huru, wa haki, wa kuaminika na unaothibitishwa kila wakati hakika unarudisha mapenzi ya watu. Ni matumaini yangu kuwa uchaguzi huu unaimarisha maisha ya kidemokrasia ya Zambia yako, unaleta ustawi zaidi kwa watu na kuwakumbusha Waafrika wenzako kwingineko kuwa hakuna lisilowezekana. Nakutakia kila la heri katika siku na miaka ijayo," alisema.
Alisema haya wakati akituma ujumbe wake wa pongezi kwa Hichilema baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa Alhamisi, Agosti 16.
Hichilema alishinda mpinzani wake mkuu, Rais aliye madarakani Edgar Lungu, baada ya kupata kura 2,810,757 dhidi ya zake 1,814,201.
Hatimaye Raila Atangaza Rasmi Atawania Kiti cha Urais 2022
Baada ya tamko la Jumatatu, Agosti 16, na tume ya uchaguzi ya nchi hiyo, wafuasi wa Hichilema walivamia mitaa ya mji mkuu Lusaka kusherehekea.
Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Zambia wa 2016, Hichilema alishindwa na Lungu na kiasi kidogo sana cha kura 100, 000.
Read ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZ4B1hY9mqZqhnJZ6osPArKCloV2vrq6uyJpkpK%2BRYrWissuaZLKZXaDCorzIrJ%2BwmV2gxKJ50ZqgrGWdpcaiesetpKU%3D