Huyu ni kiongozi wa upinzani sasa, Mbunge Ngunjiri amtania DP Ruto

- Ngunjiri amemtania DP Ruto kuwa matamshi yake siku hizi ni kama ya mtu asiye serikalini - DP amegeuka mwanablogu na mara nyingi anaonekana akiteta mtandaoni kama wananchi wengine - Licha ya kuwa waliunda serikali ya Jubilee na Rais Uhuru, DP anaonekana kugeuka na kuwa mtu mnyonge na asiye na usemi serikali

- Ngunjiri amemtania DP Ruto kuwa matamshi yake siku hizi ni kama ya mtu asiye serikalini

- DP amegeuka mwanablogu na mara nyingi anaonekana akiteta mtandaoni kama wananchi wengine

- Licha ya kuwa waliunda serikali ya Jubilee na Rais Uhuru, DP anaonekana kugeuka na kuwa mtu mnyonge na asiye na usemi serikali

Mbunge wa Nyeri Mjini Ngunjiri Wambugu amemtania Naibu Rais William Ruto kuhusu kutengwa kwake kutoka serikalini.

Ngunjiri alisema matamshi ya Ruto hivi maajuzi si ya kiongozi mwenye usemi wowote kwenye serikali ila yale ya sauti za upinzani.

Habari Nyingine: Waziri Magoha asema ni Rais pekee ana uwezo wa kuamua ni lini shule zitafunguliwa

Licha ya kuwa kiongozi wa pili kwenye serikali ya Jubilee, DP Ruto ameonekana kukosa mamlaka na badala yake kubaki kuteta mtandaoni tu kama mabloga.

Baada ya serikali kuonekana kuwahangaisha maseneta watatu kwenye suala tata la ugavi wa mapato, DP aliingia kwenye mtandao na kuchemka.

Habari Nyingine: Waziri Magoha asema ni Rais pekee ana uwezo wa kuamua ni lini shule zitafunguliwa

Ngunjiri, ambaye amekuwa kiaongoza mrengo wa Kieleweke unaomlima DP Ruto kisiasa, alimcheka na kusema ameonyesha dalili za kuwa upinzani kwenye siasa zijazo.

"Kiongozi wa upinzani? Ama ni mimi pekee nafikiri hii ni taarifa ambayo tunaweza tarajia kutoka kwa kiongozi wa upinzani na wala si naibu wa rais?" alisema DP.

"Lakini wacha niseme tumeanza kumzoea kiongozi wetu wa upinzani siku zijazo," aliongeza Ngunjiri.

Habari Nyingine: Polisi Muhororoni wawakamata vijana zaidi ya 30 wakiwa kwenye party

Licha ya kuunda serikali ya Jubilee pamoja na Rais Uhuru Kenyatta, Ruto amekuwa mnyonge kwenye serikali huku akionekana kutengwa.

Tayari wandani wake kwenye serikali wamekuwa wakiwindwa na kutimuliwa kutoka nyadhifa walizokuwa wakishikilia.

Duru pia zimearifu urafiki wake na Rais kisiasa ulififia na kilichobaki kati yao sasa ni shughuli rasmi za serikali ambapo hana sauti.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 073248269.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbIF6fZRmn66xpWK7qnnKoqann5%2Bvtm7DwGasqaGer66vtYysmKyZXaKvtrrGnmSnn6Wjt6q%2ByGaYpqyRo7aiecOpZKutpKR7qcDMpQ%3D%3D

 Share!