George Magoha ni lazima kuufanya mtihani wa COVID-19, virusi hatari

Baada ya tangazo la Rais Uhuru Kenyatta kuwa kulikuwa kumepatikana kisa cha kwanza cha mwathiriwa wa virusi vya corona, Wakenya waliingiwa na uoga na serikali nayo ilichukua hatua ya kwanza kwa kutoa amri kuwa shule zote - msingi na upili hata vyuo vikuu vifungwe.

Baada ya tangazo la Rais Uhuru Kenyatta kuwa kulikuwa kumepatikana kisa cha kwanza cha mwathiriwa wa virusi vya corona, Wakenya waliingiwa na uoga na serikali nayo ilichukua hatua ya kwanza kwa kutoa amri kuwa shule zote - msingi na upili hata vyuo vikuu vifungwe.

Pia Soma: COVID -19: Maneno 'mapya' ya Kiswahili yanayotumiwa katika janga hili

Amri hii ilifanya au kuiweka Wizara ya Elimu katika hali ya mshikemshike na kukuna kichwa. Muhula wa kwanza kulingana na kalenda ya wizara, muhula ulianza tarehe sita Januari, 6, 2020. Ulikuwa ukamilike Aprili 10, 2020.

Shule zilifungwa mapema muhula wa kwanza ambao ulikuwa uwe na wiki kumi na nne. Zilikuwa zimesalia wiki nne ambazo ni nyingi sana kwa mwalimu na mwanafunzi. Wiki hizo tayari zimeisha.

Pia Soma: 'Likizo ya Korona' kuathiri matokeo ya mitihani shuleni

Shule zilikuwa zifunguliwe kwa muhula wa pili, tarehe Mei 4, 2020 na ukamilike tarehe saba Agosti. Wiki kumi na nne vilevile.

Muhula wa tatu ambao huwa mfupi kwa wanafunzi kwa sababu ya mitihani, ulitarajiwa kuanza Agosti 31, 2020 na ukamilike Oktoba thelathini wiki nane za kusoma. Kisha mtihani wa KCPE uanze tarehe Novemba 02 hadi Novemba 4, 2020.

Nayo mitihani ya KCSE ilikuwa imeratibiwa kuanza tarehe Novemba 6, 2020 na ikamilike Novemba 30, 2020.

Pia Soma: Maradhi ya COVID-19 yazidi kuchanganya watalaam

Sasa wizara ya elimu imejipata ambapo ni lazima ibadilishe kalenda ya masomo katika shule zote nchini. Swali ni je, hizo wiki nne ambazo zilipotea zitafidiwa vipi? Na wapi? Huenda hata tukaingia katika muhula wa pili ikiwa janga hili la corona halitakuwa limedhibitiwa (Mungu atujalie heri).

Sasa wizara ya elimu ina mtihani mgumu kufanya marekebisho katika kalenda yake. Mtihani ambao wadau katika sekta ya elimu wanasubiri majibu kwa hamu na ghamu. Mungu awape hekima wanapotafuta suluhu na majibu ya mtihani huu wa 'KORONA'.

Mungu atuepushe na jangahili na atupe afya njema.

Makala haya yameandikwa na Sakwa Titus mwalimu na mwandishi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdjan16hZRmnp6nopyybrnAoKahmV2jtm64wLOgppldoMK2ssCnsJplnam2qa3NomSwmV2YvLe1w2ZocmWmnr%2B2v8hmn5qskae2b7TTpqM%3D

 Share!