- Wanane hao walikuwa wamejikinga mvua chini ya mti
- Waliojeruhiwa walikimbizwa kupokea matibabu katika hospitali ya Mkongani
Watu wawili walipoteza maisha yao Alhamisi, Machi 19 huku wengine sita wakiachwa na majeraha baada ya kupigwa na radi katika eneo la Mtsamviani, kaunti ya Kwale.
Walioshuhudia kisa hicho waliiambia Citizen Digital kwamba wanane hao walikuwa wamejikinga mvua chini ya mti.
Habari Nyingine: Serikali yawaruhusu wagonjwa wa Coronavirus kuenda nyumbani kwao Kitsuru
Sita hao ambao waliachwa na majeraha madogo madogo walikimbizwa katika hospitali ya Mkongani kupokea matibabu.
Habari Nyingine: Pasta adai alipewa ufunuo wa janga la Coronavirus 2019
Viongozi wa eneo hilo wamewaonya wakazi dhidi ya kujikinga chini ya miti wakati kunaponyesha au kukiwa na ngurumo ya radi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaYN6gJBmaWavkaW8tbHZmmSmmZmotaJ5lWaumqKVp8KptdaaZJuZkZmubsXAZqKuqJmcxKJ5zZpkq5mUnnupwMyl