Mwanamume mmoja katika kijiji cha Mwakingali, eneo la Voi anajutia hasira zake baada ya mkewe kumtema kwa kubomoa nyumba yao.
Wawili hao waliripotiwa kuwa na ugomvi wa mara kwa mara ulioishia kwa vita vikali kati yao.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Picha ya kusisimua ya Gavana Ann Waiguru akiwa shule ya upili
Habari Nyingine: Tendo la ndoa lapigwa marufuku Makueni
Licha ya kukosana na kupigana, wapenzi hao waliendelea kuvumiliana na kuishi pamoja, lakini mume wa mke husika aliteleza siku ya kiama na kuharibu uhusiano wake na mke.
Siku moja, mwanamume huyo alirejea nyumbani na kumkosa mkewe, jambo lililomfanya kupandwa na hasira.
Habari Nyingine: Pasta akatiza harusi ghafla baada ya mabinti kunengua kiuno kupita kiasi kanisani
Mwanamume huyo alianza kubomoa nyumba yao kwa kutumia jembe kutokana na hasira yake.
Mkewe alikuwa amekwenda kumtafuta mhubiri wao ili aweze kuwasaidia kutatua tofauti zao za kinyumbani aliwasili na kushangazwa kupata nyumba yake imeharibiwa huku mumewe akiendelea kuiangusha kabisa.
Kwa majuto, jamaa huyo alijaribu kumwomba mkewe msamaha lakini hakumsikiza. Alimsihi kuwa angejenga nyumba nyingine, lakini mkewe aliondoka na kwenda zake.
Habari Nyingine: Kutana na Mkenya ambaye hula mayai bila kutoa maganda
Mhubiri na watu waliokuja kutatua mzozo huo wa kinyumbani walikosa la kusema na kumfwata mwanamke huyo muda mfupi baadaye huku wakimwacha mume wake akiwa mpweke bila mahali pa kulala.
Wanakijiji ambao walivutiwa na tukio hilo muda mfupi kabla ya mkewe jamaa huyo walishangaa kwa nini jamaa huyo alibomoa nyumba hiyo kutokana na hasira.
Aliachwa akiwa amempoteza mkewe na nyumba yake na kushindwa pa kwenda wala wa kumlilia.
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Isaac Nyamwamu: Mwanamume Mkenya anayekuwa maganda ya mayai | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibYJxgpFmpKSdXZa6tbHMmmSmrZ2axKZ51aigZqOnlnqswcGopKiZXaPGtrnBmmSymZ9iuLbAzqSYp5ldo65uucizprOnXa6ubrfIp7CupZKWu6p6x62kpQ%3D%3D