- Baba anadaiwa kumuumiza na kumwacha na majeraha mwanawe akitumia bomba la plastiki
- Mtoto huyo wa darasa la sita alikuwa amekosa kumpa ripoti ya mwisho wa muhula wakati shule zilipofungwa
- Baba anazuiliwa na polisi katika Kituo cha Polisi cha Central jijini Kisumu
Mwanafunzi wa darasa la sita Kaunti ya Kisimu anauguza majeraha mabaya sana baada ya kupigwa na baba mzazi baada ya kukosa kuwasilisha ripoti yake ya mwishowa muhula shule zilipofungwa.
Polisi wanamzuilia baba yake, Hezekiah Obusebe, aliyekamatwa katika Taasisi ya Mafunzo ya Juu naTeknolijia ya Ramogi (RIAT) jijini Kisumu baada ya majirani kufahamisha polisi.
Habari Nyingine: Mwanamke akutwa akiiba TV mtaani, arekodiwa kwenye video akipata kichapo cha mbwa koko
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Kulingana na ripoti ya Citizen TV, Obusebe anazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Central mjini humo wakisubiri ushahidi na uchunguzi kukamilishwa.
Mtoto huyo anaripotiwa kupata majeraha mabaya sana wakati akiadhibiwa na baba yake ambaye alikuwa na hasira sana.
Habari Nyingine: Mtangazaji wa Ebru TV amuonyesha Eric Omondi uchi wake kwenye video, Wakenya hawaamini
Habari Nyingine: Mwanamke akutwa akiiba TV mtaani, arekodiwa kwenye video akipata kichapo cha mbwa koko
Mkuu wa kituo hicho cha polisi Boniface Mutie alithibitisha kutokea kwa kisa hicho na kwamba mtoto huyo alipelekwa hospitalini kwa matibabu na kupata fomu ya P3.
Kwa mujibu wa majirani, mtoto huyo anaishi na baba yake baada ya mama kupewa talaka zamani na baba alitumia bomba la plastiki kumwadhibu mtoto wake huyo.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibX9xfJdmmZqakWKurK3MmquwmV2gxKJ5yq6kqaGXlnquw8CnmLCdXZa5qsXEpKasmV2gwq68wGapoqifqbZuxcBmpLCho528bsPAZqSuoKWhrm%2B006aj