-Afisa wa kwanza alinaswa Rongai akitekeleza uhalifu
-Constable Kirongo alidaiwa kuwateka nyara na kuwaibia wanafunzi wa chuo kikuu
-Alipatikana na misokoto 29 ya bangi, hali iliyoonyesha alihusika katika uuzaji wa dawa za kulevya
-Afisa wa pili alikamatwa mjini Thika baada ya kutekeleza dhuluma na kutoroka
-Constable Mbogo alidaiwa kumtandika na kumdhulumu afisa mwenzake wa polisi
Maafisa wawili wa polisi walikamatwa Jumanne, Mei 29 katika maeneo tofauti kwa kuhusika na shughuli za uhalifu.
Ripoti za polisi zilizoifikia TUKO.co.ke Jumatano, Mei 30 zilisema kuwa afisa wa kwanza alikamatwa eneo la Rongai, kaunti ya Nakuru aliporejea eneo ambako alidaiwa kutekeleza wizi wa kimabavu wiki mbili zilizopita akitumia gari alilokuwa nalo.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: Ulafi wa baba wamfanya bintiye kutalikiwa dakika 15 baada ya harusi
Kamanda wa polisi katika kaunti ya Nakuru aliripoti kuwa Constable Arthur Kimathi Kirongo anayefanya kazi katika kitengo cha mbwa cha Nakuru alidaiwa kuwaibiwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Kabarak. Alikamatwa kwenye lango kuu la chuo hicho.
Mlinzi mmoja wa chuo hicho, Weldon Koima alisema kuwa gari lililotumiwa kuwateka nyara na kuwaibia wanafunzi Mei 13 lilionekana likiwa limeegeshwa katika chuo hicho.
Maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Menengai walipewa habari hizo.
OCS wa Menengai na wapelelezi kutoka ofisi ya mchunguzi wa makosa ya jinai (DCI) walielekea katika eneo hilo na kumkamata Constabe Kirongo.
Habari Nyingine: Raila Junior ashambulia wanaomtaka babake kuzungumzia ufisadi nchini
Misokoto 29 ya bangi ilipatikana katika gari hilo aina ya Nissan Sunny lenye nambari ya usajili KAU 235F.
Wanafunzi walioibiwa na afisa huyo ndio waliolitambua gari hilo. Muhsin Aden Abdi na Brian Githinji Kihiu walikuwa wameibiwa KSh 3,100 na KSh 5,000 mtawalia.
Afisa huyo wa polisi alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Menengai na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatano, Mei 30.
Jamaa aliyekuwa akishirikiana na afisa huyo wa polisi ambaye bado hajatambuliwa alitoroka na anasakwa na polisi
Habari Nyingine: Kutana na sosholaiti Mtanzania anayewapa tumbo joto Vera Sidika na Huddah
Mjini Thika, Constable Amos Njeru Mbogo anayefanya kazi katika ofisi ya mkurugenzi wa uchunguzi wa makosa ya jinai (DCI) eneo la Thika Mashariki alikamatwa kwa kumdhulumu afisa mwenzake wa polisi.
Kamanda wa polisi eneo hilo alisema afisa huyo ataadhibiwa kwenye himaya ya idara hiyo kwa kumtandika afisa mwenzake, kukaidi amri na kutumia lugha chafu kwa afisa wa polisi wa ngazi ya juu.
Atashtakiwa kwa kutatiza shughuli za uchukuzi kwenye barabara ya umma.
Inspekta mkuu wa kituo cha polisi cha Makongeni James Mwita alisema kuwa waliliona gari moja likipita eneo kusikostahili kutumiwa na gari katika barabara ya Thika kuelekea Garissa.
Habari Nyingine: Wanaume wenye wanawake wanene huishi maisha marefu, yenye furaha - utafiti
Alimuomba dereva wake asimame kutokana na alivyokuwa akiendesha gari hilo vibaya. Constable Mbogo alimgonga OCS aliyeanguka juu ya gari lingine.
Mbogo alimtusi OCS na akaondoka eneo hilo akiliendesha gari lake.
OCS huyo alimwarifu afisa wa polisi aliyekuwa na pikipiki ambaye aliyatumia magari mengine kulizuia gari la afisa huyo.
Mbogo alipogundua alizuiwa, aliondoka kwenye gari lake na kuanza kupigana na afisa huyo ambapo aliuuma mkono wake.
Maafisa wengine walifika kwenye eneo la tukio na kumkamata afisa huyo na kumzuilia katika kituo cha polisi Makongeni.
Read ENGLISH VERSION
Una taarifa motomoto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Kazi 7 mbaya zaidi duniani | TUKO TV
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibIJ0f5ZmpJqZlp7AonmRZq6aZaCkuaq%2FyGaumqORoq61w8BmorCZXaDCqcHSoqKaZZ6Wera0wKWgn61do66swdGuZK2gmaCub7TTpqM%3D