- Bintiye gavana wa Nairobi, Mike Sonko amejivunia baada ya kuonekana kwenye picha akiwa amejivika pete ya almasi kwenye kidole chake cha kati
- Haijabainika iwapo kuna mwanaume ambaye amemposa ila ni hivi tu majuzi ambapo aliweka picha ya mwanaume ambaye hakumuonyesha sura kwenye ukurasa wake wa Instagram akiashiria kwamba yuko na mpenzi
- Itakumbukwa kwamba Saumu alimtaliki mume wake mwaka mmoja uliopita baada ya tetesi kwamba hakuwa mwaminifu katika ndoa yao
Binti wa gavana wa Nairobi Mike Sonko amewaacha wafuasi wake wengi vinywa wazi baada ya kuonekana kwenye picha akiwa amejivika pete ya almasi kwenye kidole chake cha kati.
Habari Nyingine: Mambo 13 ya kushangaza ambayo wanawake Wakenya hufanya katika mahusiano yao ya kwanza ya kimapenzi
Saumu Mbuvi ambaye alimtaliki mume wake waliokuwa wamejaliwa mtoto mmoja mwaka mmoja uliopita, amekuwa akiishi nyumbani kwa babake ambapo amekuwa akilea mtoto wake.
Habari Nyingine: Lazima ‘nionje’ mpenzi wangu kabla ya ndoa - mwigizaji asema
Ni hivi majuzi tu ambapo Saumu aliweka picha kwenye ukurasa wake akiwa na mwanaume ambaye hakumuonyesha sura na kuashiria kwamba alikuwa amejinyakulia mpenzi mwingine.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
TUKO.co.ke haikuweza kubaini iwapo mrembo huyo alivikwa pete na mpenzi wake mpya au ilikuwa ni vipodozi tu.
Wafuasi wake waliachwa na maswali mengi huku wengi wakitaka kujua iwapo Saumu ameamua kuwa na mpenzi mwingine ikizingatiwa kwamba baba wa mtoto wake alishajinyakulia mpenzi mwingine tayari.
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdibH5zfZdmn66dnpmubq7Ip6uisZVitKLCwKeYZqufo7iwecCmnKmno6yubsDIs5immV2lsrWxjJqjorGfq7asw8Bnn62lnA%3D%3D