- Jamaa mmoja kutoka kaunti ya Turkana amelalama baada ya afisa mkuu wa polisi kukataa kumrejeshea gari lake linalosemekana kumgharimu KSh 1.2 milioni
- Kulingana na taarifa tulizozipokea hapa TUKO.co.ke, inasemekana gari la Simon Longolol lilichukuliwa na afisa huyo baada ya Longolol kukamatwa mwaka wa 2016
-Longoloi alidai kuwa afisa huyo mkuu amepuuza amri ya korti ya kumrejeshea gari hilo kutoka Disemba 2017
Jamaa mmoja ambaye alikuwa amekamatwa kwa makosa ambayo hakuyataja, amelalama baada ya afisa mkuu wa polisi kaunti ya Turkana kukataa kumrejeshea gari lake alilolichukua mwaka wa 2016.
Habari Nyingine: Huyu ndiye 'Mr Nakuru'; barobaro anayewazingua wanawake kwa tabasamu lake
Habari Nyingine: Mtangazaji wa Citizen TV - Jeff Koinange - ajuta kuuliza maana ya 'lamba lolo'
Simon Longolol alisema kuwa gari lake lililomgharimu KSh 1.2 milioni limeegeshwa katika kituo cha polisi tangu alipokamatwa mwaka wa 2016.
Longolol alisema alikuwa aliachiliwa kwa dhamana ya KSh 20,000 na juhudi za kupewa gari lake hazijafua dafu na haelewi ni kwa nini afisa huyo hataki kumpatia gari lake.
Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka
Habari Nyingine: John Allan Namu akiri kudanganya katika uhusiano wa kimapenzi na aliyekuwa mpenziwe
Afisa huyo anasemekana kupuuza amri ya korti ya kumtaka Longolol arejeshewe gari lake.
" Nilikamatwa mwaka wa 2016 na baadaye kesi yangu kumalizika Novemba 2017, nilirudi kortini kutaka kupewa gari langu lakini afisa mkuu wa polisi kaunti ya Turkana alikataa," Longolol alisema akiwa amejawa na hasira.
Gari hilo lilitakikana kupeanwa kwa Longolol Disemba mwaka jana lakini lingali mikononi mwa polisi huyo kufikia sasa.
Read: ENGLISH VERSION
Una taarifa moto au sakata ambayo ungependa tuichapishe? Wasiliana nasi kwa news@tuko.co.ke, mwangi.muraguri@tuko.co.ke , kwenye WhatsApp: 0732482690 na kwenye Telegram: Tuko News
Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4ZyfZhmmJ%2Bho5Z6rrfUrmSwmV2lvK210qJkmqORqa6ttcBmnpqqmWK5onnJmqSamV2iurC2wGaYpaGpmri2w8BmpJ%2BtnpzEonrHraSl