- Waziri mpya wa ardhi Farida Karoney amejipata katika hali tata huku jirani yake aking’ang’ania shamba ambalo anadai kuwa lake
- Waziri huyo alikuwa ameizingira shamba hilo kwa ua baada ya kupata agizo kutoka kwa mahakama ya Kapsabet
- Jirani yake ambaye ni mwenyekiti wa Athletics Kenya Youth Programmes Barnabas Korir pia amedai kuwa yeye ndiye mmiliki wa shamba hilo
Waziri mpya wa Ardhi Farida Karoney amejipata katika hali tatanishi siku chache tu baada ya kuteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Karoney na jirani yake wanang'ang'ania kuuhusu umiliki wa shamba katika kijiji chao.
Habari Nyingine:Diamond azidi kuwachanganya wafuasi wake, amerudiana na mpenziwe wa zamani Wema Sepetu?
Uzito wa suala hili lilidhihirika Ijumaa, februari 16 baada ya maafisa wa polisi 16 waliojihami kwa bunduki walipolivamia shamba hilo kutoa ulinzi huku wajenzi wa Karoney wakitengeneza ua.
Haya yakiendelea, Karoney alikuwa akilishwa kiapo ya afisi Ikuluni.
Keshowe alipofika katika eneo hilo, Karoney alidai kuwa alikuwa ameinunua shamba hilo kutoka kwa mmiliki wa awali, Linus Kogo, 2017 na kusisitiza kuwa ana hati miliki.
Habari Nyingine:Haya ni mataifa yaliyo fisadi zaidi barani Afrika, nambari ya Kenya itakushtua
''Kuna rekodi kutoka kwa mamlaka husika zinazoonyesha kuwa nililinunua shamba hili kulingana na sheria kutoka kwa Kogo na kumlipa Ksh 3 milioni. Wanaoshuku kuwa mimi si mmiliki wa shamba hili wako huru kumuuliza aliyeniuzia.’’ Karoney alisema.
Jarida la TUKO.co.ke lilimnukuu Kogo akieleza kuwa aliliuza shamba hilo lote kwa Kwa Karoney, 2016 na kuwa alimaza kumlipa fedha zote.
Habari Nyingine:Sahau Inspekta Mwala, huyu ndiye mcheshi mfupi zaidi nchini Kenya?
''Mimi ndimi niliyekuwa mridhi pekee wa Maria Cheptile ambaye alikuwa na hati miliki ya shamba hili kabla kufariki. Nilienda kortini 2015 na mwaka moja baadaye niliyaweka mashamba yote kwa jina langu na kupata hati miliki. Baadaye nililiuza shamba hili kwa Karoney ambaye sasa ndiye mmiliki.'' Kogo alinukuliwa.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2Bvzmeinmdia4N6fZJmrpqymae2brnPsphmr5FirrOwx6Jkn5minrGiecqaqaimla56osbOs5inoZFiwKmtzJuYZqaRYreqvsCnoGaxkaCyb7TTpqM%3D