Sijaolewa kwa sasabu uliniroga Mpenzi wa zamani wa jamaa adai

-Jamaa mmoja ameshangazwa na matamshi ya mpenzi wake wa zamani kuwa alimroga na kumfanya akose mpenzi wa kumuoa -Jamaa huyo alidai kuwa waliachana na kipusa huyo alipogundua kuwa alikuwa na mipango ya kando

-Jamaa mmoja ameshangazwa na matamshi ya mpenzi wake wa zamani kuwa alimroga na kumfanya akose mpenzi wa kumuoa

-Jamaa huyo alidai kuwa waliachana na kipusa huyo alipogundua kuwa alikuwa na mipango ya kando

-Inadokezwa kuwa jamaa alioa lakini kipusa huyo ambaye humpigia simu mara kwa mara hajawahi kuolewa, hali inayomfanya kumwelekezea lawama mpenzi wake wa zamani

Jamaa mmoja yuko katika njia panda baada ya mpenzi wake wa zamani kudai kuwa alimroga na kumfanya akose mpenzi mwingine.

Jamaa huyo ambaye hakutaja aliko alisema kuwa waliachana na kipusa huyo miaka kadhaa iliyopita. Yeye alibahatika na kumpata mpenzi mwingine na akamwoa.

Jamaa huyo anasema kuwa mpenzi wake wa zamani hajaolewa na hajawahi kuwa na mpenzi mwingine, jambo ambalo limemfanya kumlaumu jamaa huyo kwa kudai kuwa alimwendea kwa werevu na kumroga.

Habari Nyingine: Pasta ‘mla kondoo’ aanikwa na mkewe!

Jamaa huyo ambaye alituma ujumbe wake kwa TUKO.co.ke alisema kuwa binti huyo anaelekea kumharibia uhusiano wake kwani anampigia kila mara na kutishia kusambararisha uhusiano wake na mpenzi wake wa sasa.

“Sasa amekuwa akinipigia simu kulalamika eti nilimroga asiwahi kuolwea na anajaribu kunilazimisha tuwe na uhusiano wa pembeni. Nifanyeje?"

Jamaa huyo aliyewaomba wana TUKO.co.ke kumfaa kwa maoni hakufichua ikiwa mpenzi wake wa sasa anajua balaa iliyopo kutokana na binti huyo au ikiwa walikuwa wakikutana na mpenzi wake wa zamani.

Habari Nyingine: Jamaa wawili watwangana waking’ang’ania kipusa mgeni kwenye ploti

Haya ni baadhi wosia aliyopewa na wasomaji wa TUKO.co.ke:

Una maoni? Una taarifa ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoV1go9mqqKikaS5psPAZqKwmV2orrStwa5krqSZo7azu8aaZKaolaPHqnnWmmSzmZ2Wu6p51ppko5mdlq5urcOaoGegpKK5

 Share!